Sunday, April 18, 2010

Malekezo ya mwanzo kabisa ya kutengeza wavuti(Introduction)

Watu wengi wamekuwa wakifikilia jinsi ya kutengeneza wavuti, wamekuwa wakijaribu kutengeneza website Tovuti(wavuti??? Kiswahili kigumu) lakini wanashia njiani kwani wanakuwa hawajui nini wanatakiwa kufanya kwanza kabisa kabla ya kutengeneza website zao.
Hatua ya kwanza kabisa ya kutengeneza website (haijalishi kama wewe ni webprogramer au hujui chochote kuhusu programing) au  mambo muhimu ya kuzungatia kabla ya kuamua kufungua au kutengeneza website .
1. Weka mipango Kabla(make a plan).
    Kila kitu hapa ulimwenguni kikifanyika bila ya kuwa na mpangilio huwa ni kibaya au huwa hakivutii kama mtu aliyekaa chini na kupangilia kazi yake. Kwa hiyo kabla hujaanza kutengeneza website unatakiwa kupanga vizuri kuhusu website yako, unatakiwa kujua itakuwa inahusu nini, kama ni kuhusu company yako, au ni ya  kufurahisha jamii. Umuhimu wa kupanga ni kwamba utaweza kujua vizuri hasa wakati unafanya hosting(kuhifadhiwa mafaili yako) kujua kuwa ni nani anatoa hosting services nzuri kwa ajili ya website yako au nani ana server(computer maalumu ya kutunza mafaili yako ya website) nzuri kwa ajili ya webiste yako pia kuweka plan kutakusaidia kuchagua a programmer (injinia wa kutengeneza website) kama ukiwa hujui kabisa kuhusu kutengeneza website Pia itakusaidia kujua Gharama za pesa au matumizi ya website yako. Kwenye blog hii nitatoa maelekezo ya kumsaidia mtu anayejua basic skills za website sio lazima ukawa professional ndio uweze kutengeneza professional website ukinifuatilia kwa makini maelekezo kwenye blog hii utaweza kutengeneza website kama professional. Ninasistiza kuwa kama utataka kujua viziri jinsi ya kutengeneza kupitia blog hii lazima ujifunze au uwe na ufahamu wa msingi(basic knowledge) wa HTML, au CSS ili uweze kutengeneza website yako.
2. Ubunifu(Creativity)
     Kuhusu ubunifu ni kwamba watu huwa hawafikilii kuhusu kuwa wabunifu katika kazi ya kutengeneza website, Utakuna mtu anakurupuka tu na kuweka kila kitu anachojua kwenye website na kupanga anavyotaka kisha akaita hii ni website au hii ni blog ni sawa ila ukifika wakati wa kufanya mashindano ya biashara au kuweza kupata trafic(watu wanaotembelea website yako kwa mwezi) ya kutosha hapo itategemea wewe umeweza vipi kufanya ubuifu au website yako imetengenezwage, pia kama unategemea kupata wadhamini wa kuweka matangazo kwenye website yako basi itategemea ni jinsi gani wewe umeweza kubuni website yako na kuitengeneza vizuri ili kila anayekuja kupitia website yako aweze kuduri tena na kuangalia nini kilichomo ndani ya website yako.
  Watu wanaweza kusema kuwa Ubunifu(creativity) huwezi kusomea maana ni kipaji cha mtu , ni kweli kabisa na ila ni kwamba unaweza kukiendeleza kipaji chako kama utaweza kuwasoma(hahaha kiswahili cha kisasa) nina maana kama utaweza kujifunza kutoka kwa  baadhi ya website ambazo ni nzuri na pia hata bloggers wazuri (maarufu) kama Michuzi Tanzania.
  Pia Ubunifu huu unachangia hata jinsi unavyoandika makala za website yako na ni  jinsi gani ulichokiandika kinavyovutia watu, haka kama unategemea kupata pesa kupitia website yako basi unatakiwa kuangalia kwa umakini mkubwa jinsi unavyoandika kwenye website yako na jinsi ulivyopangilia maandishi yako, kama hujui kuandika vyema ni vizuri ukapitia kwenye mtandao kwani kuna watu wengi wanaelekeza jinsi ya kuandika kwa kuvutia.
3.UVUMILIVU
Ninapenda kuwa muwazi katika swala hili la kutengeneza website , kikubwa unachotakiwa kuwanacho ni Uvumilivu(hahaha…ni kama wakristo wamekuwa kwa muda mwingi wakingojea masihi ambaye ni kristo yesu na sasa ni miaka zaidi ya 2000 bado hajaja…wow ni uvumilivu wa hali ya juu, hahaha… ni ninaamua kukufanya walau utabasamu maana naona umekuwa makini sana) zao. Kweli ni kwamba watu wengi siku hizi wanatengeneza hela nzuri sana kupitia website zao. Sasa kwa hili swala uvumilivu ni kitu cha msingi sana na cha muhimu sana. Ninazungumzia uvumilivu ni kwa wale wanaotaka kupata pesa kupitia website(wovuti(tovuti???? Ninachanganyikiwa na kiswahili))



Kwa sasa sitazungumzia swala hilo la kupata pesa kupitia mtandao ila nitalizungumzia mara baada ya kufika karibu na mwisho wa maelekezo haya katika blog hii…






4. Furahi kwa kuweza kupata maelekezo haya..hahahah...mimi ni mcheshi kidogo..hahaha

Pia enjoy huduma hii

8 comments:

  1. But in general, the site is well crafted and good organized, the design is eye-catching and the color pattern is very attractive.

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa maelezo yako,je kama nina website ya company na hiyo website nikafungua ID's kwa kila mfanya kazi na server ipo marekani nitaweza kuona kila wanachofanya kwenye id zao.ningefurahi kama utanijibu kwenye email yangu.
    iman mahmud
    iyman44@yahoo.com

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu, Habari bwana, Samahani nilikua busy sana sikuweza kuona kama ulikua umewema comment hapa, sawa kaba bado hujapata jinsi ya kufanya nitakuandikia email, nitakueleza. kama umepata niambia ili niendelee na kazi nyingine....SAMAHANI SANA KUCHELEWA KUKUJIBU

      Delete
  3. Dailyitnewsbd
    But it general... The site is well & good....

    ReplyDelete
  4. Nataka nijue jinsi ya kuanza kufungua blog mgayac9@hmail.com

    ReplyDelete
  5. Nataka nijue jinsi ya kuanza kufungua blog mgayac9@hmail.com

    ReplyDelete
  6. Nataka kujua jinsi ya kufungua blog yangu

    ReplyDelete
  7. Habari yako bro, nakushukuru sana kwa kutupa maelekezo mazuri ya jinsi ya kufungua website or blog ila kwa upande wangu nilikuwa naomba maelezo zaidi kwa upande wa blog afu kama pia hutojali ata website pia kwa sababu naitaji niwe navyo vyote viwili kwa jili ya mambo yangu ya kimaendeleo kwahyo nitashukuru sana kama utanisaidia ombi langu bro.

    ReplyDelete

please do not use abusing language, Tafathali tumia Lugha safi(Nzuri)