DOMAIN kwa lugha yetu ya taifa kutafsili neno hili lina mgogoro maana kamusi inasema maana ya neno hili ni ENEO hahahahha…Ok tuachane na Kiswahili Domain tukiwa tunazungumzia maswala ya website tuna maaninasha ni Jina au anuani yako ya website hapa ninamaanisha kitu kama www.tovutiyako.co.tz au www.websiteyako.com nafikili hapo mtu anaweza kunielewa kirahisi.
Pia HOSTING kwa Kiswahili sijapata maana yake(japokuwa mimi ni mmoja kati ya watu wanaosisitiza matumizi ya Lugha ya Kiswahili katika elimu ya Tanzania hasa ya chuo kikuu nitatoa sababu kwenye blog nyingine nitakapo kuwa ninazungumzia maswala ya umuhimu wa kusoma kwa lugha yako) ila hili neno lina maanisha mahali(kampuni) yenye compyuta(kichakato) maalum kwa ajili ya kutunzia mafaili ya wavuti(website) kwa rugha nzuri ni seva (web-server) au kama ni computer yako ya nyumbani basi wewe utakuwa ni host wa website yako ila pia inatakiwa kuwa na sifa ya kuweza kuchapisha au kuyaweka mafaili yako ili yaweze kupatikana kwenye mtandao(to publish online).
Sasa kabla ya kuanza kutengeneza website yako unahitaji hivi vitu muhimu viwili viwe tayari ili uweze kuanza kazi ya kutengeneza website yako.
DOMAIN NAME
Kama nilivyokwisha kueleza hapo juu DOMAN NAME ni address ya website yako ambayo inawezesha watu wengine kuweza kufungua mafile yako kupitia mtandao. Sasa jina hili unaweza kulipata kupitia makapuni mbali mbali ambayo yanatoa huduma hii, sio kwamba mtu yeyote anaweza kuandika jina lake analotaka bila ya kufuata utaratibu, ni lazima kuwasiliana na makampuni yanayotoa majina ili uweze kusajili jina la tovuti yako na kuweza kupewa anuani yake(I.P address) na kuweza kutambulika kuwa website hii ni ya nani nayupo wapi pia mawasiliano yake. Unaweza kwenda kwenye kampuni kama http://www.godaddy.com/ au unaweza kutafuta kupitia search engine kama google, yahoo au msn na ukapata makapuni mengi sana yanayotoa huduma hii ya Domain. Pia kuna baathi ya makampuni yanayotoa huduma hizi zote mbili kwa wakati mmoja na ni kwa gharama nafuu, kama www.hostgator.com na mengine mengi sana. Pia kuna makapuni yanatoa huduma hii bure ila sitapenda kuelezea sana haya ya bure maana kuna hasara nyingi sana na mtu anaweza kuja kunilaumu kuwa nilimwambia kitu kilichomwingizia hasara, ila kama unapenda kuyajua ni vyema ukafanya utafiti wa kutosha kabla ya kuweza kujisajili nayo, pia yawezekana kuna watu wanaweza shindwa kutofautisha kati ya Domain name na sub-domain name, kwani kuna makampuni mengi yanatoa sub-domain name, hakuna shida zote ni anuani ila shida moja kwenye sub-domain ni wewe unakuwa kwenye mtandao kupitia jina la mtu mwingine(sub-domain) hautaweza julikana pia hutakua na haki yeyote ya umilikaji wa jina hilo hivo itakuwa vigumu kwako kuweza kupata wadhamini wa kutosha ili kuweza kupata fedha. Ninaposema sub-domain nina maanisha domain ambayo inapitia kwenye domain nyingine kwa mfano jina la blog hii ni www.wovuti.blogspot.com , sasa hapa domain iliyosajiliwa ni www.blogspot.com, na www.wovuti.blogspot.com ni sub-domain. Sasa mwenye haki zote za website ni aliyesajili jina la www.blogspot.com.
Angalizo wakati wa kusajili jina ni kwamba unatakiwa kuwa umekwisha andaa majina zaidi ya matatu kwa ajili ya website yako kwani kuna wakati ukakuta watu wengine walisha chukua jina lako hivyo ni vyema kuwa na majina mengine. Pia ni vyema ukawa na data za kutosha.
WEB HOSTING
Hii nayo pia kama nilivyokwisha kuongelea hapo juu ni kwamba hufanywa na kampuni ambayo ina web seva (web-server) na inatoa huduma za ku-host wavuti, Huduma hii hulipiwa kulingana na matumizi yako au uhitaji wako, ila kuna makampuni mengi sana yanatotoa huduma za hosting na kwa bei nafuu sana, Sasa unatakiwa kujisajili na kampuni moja wapo kama huna web-server kwenye compyuta yako (Mungu akinisaidia nitaandaka pia jinsi ya kutengeneza home server na hata kama una small network kazini kwako basi unaweza kutengeneza ‘webserver na kuweza kupatikana kupitia mtandao (I.P-site)) , pia kama kawaida huduma za bure zipo palepale, kuna makampuni mengi sana yanaotoa huduma za bure kabisa ila siwezi pia kuzungumzia hizi maana kuna matatizo yeke na limits nyingi sana, ila kama unapenda basi ni vyema uwe mwangalifu na kujua kuwa unachotakiwa kufanya kabla ya kuingia kwenye hizi za bure, pia hata usalama wa website yako sio wa kutosha kama mtu anayetumia huduma za kulipia.
Mambo ya muhimu ya kuzingatia wakati wa kutafuta kampuni ya kijisajili nayo ni kama ifuatavyo:-
1. Unatakiwa kujua speed ya seve(server speed) ninamaaninisha sifa za seva au CPU clock, kwani ili website yako iwe na speed nzuri ni lazima seva unayotumia iwe na speed nzuri kama tunavyojua ukiwa una faili Fulani kwenye computa yako kama compyuta yako haina speed nzuri basi ni kwamba hilo fili lako litachelewa sana kufunguka, ni sawa kabisa na web seva, kama host machine haina speed ya kutosha basi tovuti yako itakuwa haia speed nzuri wakati wa kufunguka.
2. Ni vizuri kuangalia Host wako anakupa Bandwidth ya ukubwa gani, ninaposema bandwidth ninamaanisha uwezo wa kusafilisha data kwa sekunde kutoka kwenye web seva mpaka kwenye web-browser (Vilambaza) kwenye compyuta ya mtu anyefungua tovuti yako,(data transfer per second) Hoster wengi wanatoa uhuru mkubwa wa kusafilisha data , maana yeke nini ninaposema uwezo wa kusafilisha data, hii inaaanisha kuwa uwezo wa tovuti yako kuweza kupatikana kirahisi pale mtu anapoitafuta.
3. Unatakiwa pia kuangalia speed ambayo host wako atakuunganishia nayo, kwani kama kakuunganishia kwenye speed ya taratibu basi tovuti yako itakuwa inafunguka taratibu sana, na hapo kutakuwa kuna shida sana. Kwa sasa speed nzuri ni 100Mb/s
4. Unatakiwa kuangalia disk space, unatakiwa kuangalia host wako atakupa nafasi kiasi gani, hii sio muhimu sana kama unatengeza tovuti ndogo, ila kama unatengeza tovuti kubwa na yenye mambo mengi kama watu wanaweza kuweka picha zao, kuna program za kuchat, kuna miziki humo, basi tovuti kama hii ni vyema kuangalia unapewa ukubwa wa nafasi gani, ila hii inategemea sana na plani yako.
5. Unatakiwa pia kuangalia gharama za kufanya hosting sinazotolewa na kampuni inayoku-host, gharama zinatofutiana kulingana na kampuni pia na plani yako, pia gharama hizi hupungua pindi unakapo kufanya mkataba wa muda mrfu kama miezi 36 na kuendelea basi utapunguziwa gharama.
6. Angalia kwa umakini mkubwa Maongezeko ya gharama au gharama zilizojificha kama vile, kuna baadhi ya hosters wanaongeza gharama za kukuandalia seva, pia gharama bandwidth ya ziada, au kama kukuongezea huduma kama viunganishi mbalimbali vya tovuti, kwa hiyo ni vyema kabisa kuwa mwangalifu
7. Pia ni vyema kuangalia kwa umakini aina ya huduma ya barua pepe ambayo host anaitoa kabla ya kuchagua nani awe host wako,angalia kama ni web-based na pia wanatoa barua pepe ngapi, je wanatoa huduma ya auto-response, au forwarding, je wanatumia pia POP3, IMAP na SMTP zinapatikana? Unaweza kujiuliza kwanini e-mail ni muhimu wakati unaweza kutumia parua pepe yako ya yahoo, hotmail, gmail na nyingine nyingi, sawa unaweza kutumia lakini tovuti yake ni kwamba tovuti yako itaonekana si ya kitaalamu kama utatumia hizo parua pepe, unapotengeneza tovuti yako ni vizuri mawasiliano yote yanayopitia kwenye tovuti basi lazima na mawasiliano ya parua pepe yawe yanafanana na tovuti yako.
8. Pia angalia kama host wako anatoa huduma ya vionganishi vinavyokusaidia wewe kuweza kutawala tovuti yako kama vile control panel, hiyo lazima iwepo kwenye plani yako ya tovuti utakayo lipia, vitu kama menejimenti ya mafaili, Script Auto installer, Control panel ni moja ya vitu muhimu sana na ma webmaster wengi wanavipenda sana viwepo kwani vinasaidia kuweza kutawala tovuti yako kirahisi, inaatoa urahisi wa kuweza kuweka mafili yako kwenye mtandao kwa urahisi ,pia kuweza kuyameneji bila ya shida, Barua pepe zote unaweza kuziona kirahisi, pia database unaweza kuimeneji hapo kwenye control panel na unaweza kufanya kwa muda mchahe sana na kwa kubofya bofya tu.
9. Pia angalia kama host wako anatoa Script installation za bure kama vile joomla, Mambo, Wordpress, ExpressionEngine hii sio ya bure ila inatoa nafasi kubwa ya kuweza kutengeneza wavuti za kitaalamu zaidi, na pia kuna nyingine ya kikorea ambayo kwa kweni ni nzuri sana kwa mainjinia wavivu kama mimi basi hiyo kwa dakika kadhaa unaweza kuwa tayari na tovuti yako. Sasa ni vyema kuangalia kama host wako anatoa hudumma kam hizo, kwani ni muhimu kwa mtu asiyejua kutengeneza au asiyejua Lugha za kompyuta za kutengeneza tovuti.
10. Angalia pia kama host wako anatoa database na anaruhusu kufungua akaunti ngapi za database, Kwa ajili ya kutunza data na kama tovuti yako inaruhusu watu kuweza kufungua akaunti za kuweza kuweka maoni yao sasa itahitajika kuwa na database ya mysql, angalia kwa host wako anatoa huduma gani ya database.Pia angalia kama kuna myphpadmin hii ni njia rahisi sana ya kuweza kumeneji data base yako.
11. Pia angalia kama host wako anatoa sub-domain na anatoa ngapi ila uweza kuongeza website nyingine ndani ya website yako.
12. Na mwisho kwa mawazo yangu mimi ni Huduma kwa mteja, angalia kama kampuni yako ya kuhost inatoa huduma kwa mteja na ni kwa muda gani , nzuri ni kwa muda wa masaa 24, kwani kuna wakati mambo yanaweza kwenda vibaya kwenye seva na unahitajika haraka kutoa huduma fikili kama unafanya biashara kupitia mtandao, sekunde moja ni kubwa sana kwani unawea kukosa pesa nyingi sana ndani ya sekunde moja. Kwa hiyo ni vizuri kuwa na host anayetoa huduma masaa 24 na anatoa kwa mkataba gani ni nbure au unalipia.
Sasa kwa wale wanaotumia free server huwa wanakosa huduma hizi nyingi ndio maana sitaki kuzungumzia kuhusu huduma za bure, na pia kumbuka siku zote bure ni gharama, kwani ukitumia pesa kidogo utaweza kuokoa mambo mengi kuliko kutegemea za kupewa bure, Hakuna shida kwa mtu anayetengeneza tovuti ya familia au yak wake mwenyewe ila kama ni ya biashara au ni ya ofisini kwako au itahusu mwingilino wa watu wengi ni vizuri ukatumia huduma za kulipia maana zinakuwa ni zakutegemewa kuliko huduma nyingine yeyote.