KUJENGA WAVUTI

TOFAUTI KATI YA WAVUTI NA BLOGU (Website VS Blog)


        Kuna Tofauti kubwa kati ya Wavuti (Website) na Blogu (blog) ila zote zipo kwenye kundi moja la wavuti , Kwanza kabisa nianze kuelezea Blogu, hii ni aina ya wavuti ambayo inalenga hasa kwa ajili ya habari na matukio ya papo kwa hapo, blogu hazina mpangilio kamili wa wa habari zake, mtu anaweza kuandika chochote kulingana na dhumuni la blogu yake. Pia blogu yenyewe inatabia moja kila unapoongeza habari au dokumenti yako basi hujipanga juu ya ile ya zamani na kuipeleka ya zamani chini, ndio maana nimesema kuwa hakuna mpangilio kamili wa mambo yaliyomo nadani ya blogu. Kama ukiangalia blogu nyingi ni kwamba kila kimachoandikwa kinasukuma kile kilichokuwepo chini , ninaweza kusema ni maalumu kwa habari mpya za kila wakati.

        Wavuti yenyewe ina mpangilio mzuri wa maudhui na mambo yake yote yamepangiliwa vizuri ili kumuwezesha msomaji kuweza kuelewa dhumuni la wovuti, pia maudhui yake hayabadiliki sana kila wakati ingawa kunaweza kuwa na ukurasa mmoja ambao unaweza kuwa unabadilika kila wakati kwa ajili ya kupashana habari mpya, Kurasa za wovuti zipo kwenye mpangilio mzuri kumuwezesha mtumiaji kuweza kutembelea kurasa mbali mbali bila ya shida yeyotena na kwa urahisi, pia mwenye wovuti anakuwa na nafasi kubwa ya kuitawala wavuti yake kama atakavyo kulingana na dhumuni la wavuti yake, anaweza kuweka amri zake na anaweza kuruhusu nani aangalie nini na nani asiangalie, Pia wovuti inakuwa na mvuto tofauti, na hapa ndio ninasema kuwa kazi ya sanaa inatakiwa kwani bila ya sanaa kupata mvuto sio rahisi na watu wengi hawataweza kutembelea wavuti yako, ni vizuri ukawa makini sana kuangalia ni nini watu unawowaandikia wanataka, na jambo gani lina mvuto wa kutosha kuleta watu wengi kwenye wovuti yako.

       Kabla sijazungumzia kutengeneza wavuti pia ninapenda kuzungumzia kidogo wavuti za jamii kama http://www.facebook.com/ , http://twitter.com/ (ingawa watengenezaji hawasema kama ni wavuti ya jamii ila kwangu ninaona kuwa inaangukia kwenye wavuti za jamii), http://www.hi5.com/ , na nyingine nyingi sana ambazo unazijua, hizi ni wavuti kama nyingine ila ni maalumu kwa ajili ya kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya mtu na mtu, au jamii Fulani ni tofauti na wavuti ninazozizungumzia hapa, hizi kama tunavyojua mtu anaweza kuweka piacha na kuandika chochote na kikasomwa na watu wengi kwa muda mfupi na sehemu nyingi sana.


KUTENGENEZA WAVUTI(Creating your website)


Hapa nitaendela muda ujao, ila kaa mkao wa kula kwani ninakwenda kushusha nodo za nguvu na zinazooweza kumuwezesha mtu kutengeneza wovuti bila ya kujua vizuri lugha za kompyuta